IBADA YA UPEPO WA KISULISULI MLIMA WA MOTO, MAMIA WAJITOKEZA

IBADA YA UPEPO WA KISULISULI MLIMA WA MOTO, MAMIA WAJITOKEZA

Video Channel: MCL Digital

Dar es Salaam. Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameendelea kufurika kwenye kanisa la Mlima wa Moto yanakofanyika maombezi maalum kwa ajili ya kuomba ndoa kwa wanaotamani kuingia kwenye taasisi hiyo.

Mwananchi imeshuhudia idadi kubwa ya waumizi waliojitokeza kwenye ibada hiyo iliyopewa jina Upepo wa Kisulisuli.

Mmoja wa wahudumu kanisani hapo ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake amesema ibada ya leo imehudhuriwa na watu wengi kuliko ilivyo kawaida.

“Hili suala la upepo wa kisulisuli kwetu ni kawaida ila naona watu wametafsiri walivyoelewa wao, muitikio ni mkubwa mno, sura nyingi naona mpya,”


“Kama ambavyo mama alisema leo yanafanyika maombi mazito kwa wanaohitaji ndoa, wale wenye haja kweli, watu wasifikiri wanaweza kuja kujipatia wanawake kwa urahisi hapa,” amesema mhudumu huyo

Tags:
IBADA YA U
Loading...